February 28, 2018

Ajirusha baharini kina kirefu Akiwa Safarini Kwenda Zanzibar

Mwanaume mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika amejirusha baharini kutoka katika boti ya Azam iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar Jumatatu, katika eneo linalohisiwa kuwa na kina kirefu.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana inaonyesha boti hiyo ikiwa imesimama eneo ambalo mwanaume huyo alijirusha huku watu wakijadiliana namna ya kumwokoa.

Tukio hilo limeelezwa kufanyika katika eneo la Bahari ya Hindi "ukishapita Msasani" ambako kuna mkondo wa maji unaodhaniwa kusababishwa na kina kirefu cha maji.

Waliojeruhiwa kwa Risasi Maandamano ya CHADEMA waachiwa kwa Dhamana

Watu watatu wanaodaiwa kuwa wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali.

Hata hivyo, watu hao watatu wameunganishwa katika kesi ya wafuasi 28 wa CHADEMA ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyipita.

Magazeti ya Leo Jumatano ya February 28

Upasuaji Wa Kihistoria Wafanyika Moi Kwa Mafanikio

Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa  Muhimbili  (MOI) kwa kushirikiana na Madaktari wa Hosipitali ya BLK  India jana  wamefanya upasuaji maalum wa mgongo kwa kutumia matundu (Minimal Invasive Spine Surgery) kwa mgonjwa aliyedhoofika uti wa mgongo.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa

Washirika Wa Maendeleo Waahidi Kushirikiana Kwa Karibu Zaidi Na Tanzania Kuleta Maendeleo

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) imekubaliana na Washirika wa Maendeleo kurejesha uhusiano wa karibu na wenye tija ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka Mitano pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanziba (MKUZA III).

Hayo yamebainishwa mjini Dodoma na

Atiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Soli Mkanzabe (24), mkazi wa mtaa wa Nyegezi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.

“Inasemekana mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake.

February 27, 2018

Diamond Akabidhiwa Rasmi Leseni ya Wasafi TV na Wasafi Redio

Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi TV’.

Diamond amevuka maji na kuzipata leseni zake visiwani Zanzibar ambapo alikabidhiwa na Wizara ya Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.

Freeman Mbowe na vigogo wengine wa Chadema waripoti polisi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jumatatu Februari 27, 2018 Mbowe amesema wamekwenda kuripoti kuitikia wito wa Polisi.

Amesema katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji hatakwenda kwa kuwa yupo nje ya nchi na atakaporejea atakwenda kwa kuwa hawana sababu ya kugoma.

Polisi yawashikilia watu 10 kwa mauaji diwani wa Chadema Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa diwani wa Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

DPP akata rufaa hati ya kuzuia dhamana kukataliwa

Mkurugenzi wa Mashtaka DPP amekata rufaa kupinga uamuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu, Firmin Matogoro wa kukataa hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa Antonia Zakaria na Timoth Kilumile wanaokabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 3/2018 walifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza Januari 17 mwaka huu.

November 21, 2017

The Highest Paying Reward App ever! Make money quickly by downloading apps

Try BigCash: The Highest Paying Reward App ever! Make money quickly by downloading apps and games.The Best part is you can Exchange 2500 Points for $15 Paypal Cash or Amazon, GooglePlay, iTunes or Other Gift Cards.
Please Input My Invitation Code jypllr9u after installation, and you will get an extra 70 Credits From Me! You can Download it from Google Play here
https://goo.gl/xtDLEk

October 27, 2017

AGNEZ MO - Damn I Love You

Music video for Damn I Love You performed by AGNEZ MO.
Kupata Video hii bonyeza Download sasa uweze kupata.

October 24, 2017

Harmonize-Nishachoka Official video