
Hata hivyo, watu hao watatu wameunganishwa katika kesi ya wafuasi 28 wa CHADEMA ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyipita.
Washtakiwa
hao watatu walisomewa kosa lao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Godfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita.
Wakili Mwita aliwataja washtakiwa hao watatu kuwa ni Isack Ng’aga, Erick John na Aida Olomi.
Wakili
Mwita amedai washtakiwa hao, March 8, 2018 wataunganishwa na wenzao 28,
ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita.
Kwa
pamoja wanadaiwa kuwa February 16, 2018 huko Kinondoni katika eneo la
Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
walifanya mkusanyiko usio wa Halali kinyume cha sheria.
Inadaiwa kuwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha Taharuki kwa wananchi.
Washtakiwa
wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana kwa kila mshtakiwa
kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini ahadi ya Shilingi Milioni 1. 5 na
wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha
mahakama. Upelelezi bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi March
8,2018.