Kamanda
wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao
wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani.
Lwena
aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali
za mwili wake akiwa nyumbani kwake Februari 22, 2018.
Matei
amesema kwa sasa majina ya watuhumiwa hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu
uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya upepelezi kukamilika.
Awali,
katika taarifa yake kwa nyombo vya habari kamanda Matei amesema mauaji
hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa kata hiyo, Kennan
Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016.
Amesema
mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku kadhaa aliuawa.

Amebainisha kuwa eneo hilo lina migogoro ya muda mrefu ya mashamba na watu wengi wameuawa katika mazingira yanayofanana.
“Tunaendelea
na uchunguzi wa kina katika eneo lile la Namwawala na kata za jirani
ili kubaini hao wanaoendesha haya mauaji na wote watachukuliwa hatua za
kisheria,” amesema Matei.