Akizungumza
na waandishi wa habari leo mchana Jumatatu Februari 27, 2018 Mbowe
amesema wamekwenda kuripoti kuitikia wito wa Polisi.
Amesema
katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji hatakwenda kwa kuwa yupo
nje ya nchi na atakaporejea atakwenda kwa kuwa hawana sababu ya kugoma.
Februari 20,2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.
Wito
huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.
Akwilina
aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa
ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari amesema wana taarifa kuwa watakamatwa na kwamba kuna mpango wa kubambikiziwa kesi.