
Kwa
mara ya kwanza, washtakiwa katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba
3/2018 walifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza Januari 17
mwaka huu.
Washtakiwa
hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama na
kujimilikisha mali Chama cha Ushirika cha Nyanza (NCU) na kuisababishia
Serikali hasara ya zaidi ya Sh10 bilioni.
Baada
ya kusomewa mashtaka, wakili wa upande wa mashtaka Seth Mkemwa
anayesadiana na Shadrack Kimaro aliwasilisha hati ya kiapo ya DPP kuzuia
dhamana kwa kile alichoeleza ni kulinda maslahi ya Taifa na usalama wa
washtakiwa.
Baada
ya
kusikiliza hoja za upande wa utetezi unaowakilishwa na wakili Deocles Rutahindurwa, Jaji Matogoro uliitupilia mbali hati hiyo akisema haina uhalali mbele ya macho ya sheria kwa sababu imetoa hoja za jumla bila kueleza maslahi ya Taifa inayolindwa wala watakaowadhuru washtakiwa wakiachiwa kwa dhamana.
kusikiliza hoja za upande wa utetezi unaowakilishwa na wakili Deocles Rutahindurwa, Jaji Matogoro uliitupilia mbali hati hiyo akisema haina uhalali mbele ya macho ya sheria kwa sababu imetoa hoja za jumla bila kueleza maslahi ya Taifa inayolindwa wala watakaowadhuru washtakiwa wakiachiwa kwa dhamana.
Katika
uamuzi wake, Jaji Matogoro alikubaliana na upade wa utetezi kwa kusema
DDP ametumia vibaya madaraka yake kuwasilisha hati hiyo kwa sababu kwa
sababu anajua haiwezi kuhojiwa mahakamani ndio maana hakubainisha
maslahi ya Taifa inayolindwa.
"Haiingii
akilini namna gani usalama wa unavyotishiwa wala nani wanaoutishia
wakati wameishi mitaani bila kudhurika tangu mwaka 2002 wanapodaiwa
kutenda makosa hayo," alisema Jaji Matogoro katika uamuzi wake juzi.
Shauri
hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa leo Februari 27 baada
ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika,
lakini lilipoitwa ndipo wakili Shadrack alipoieleza mahakama kuwa DPP
amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kutupa hati ya kuzuia
dhamana.
Jaji Matogoro ameahirisha shauri hilo hadi kesho Februari 28 rufaa hiyo ya DPP itakaposikilizwa.