
Kwa
Mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Taasisi
hiyo Jijini Dar es Salaam, Upasuaji huo umefanywa kwa mafanikio makubwa
ukiwashirikisha Madakatari Bingwa wanne wakiongozwa na Profesa Joseph
Kahamba wa MOI na Dkt. Puneet Girdhan kutoka hosipitali ya BLK.
Taarifa
hiyo imebainisha kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa
muda wa masaa manne ambapo pamoja na upasuaji huo, MOI imeanzisha
huduma za upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu ( Athroscopy ).
“
Tayari wagonjwa 300 wameshafanyiwa upasuaji wa magoti kwa njia ya
matundu kwa ufanisi mkubwa na wagonjwa wengine wameendelea kunufaika na
huduma hii” Inasisitiza sehemu ya Taarifa hiyo
Kutokana
na mabadiliko ya teknolojia ya matibabu, upasuaji wa kupanua njia za
mishipa ya fahamu na kuimarisha uti wa mgongo kwa nyenzo za kisasa
umeshika hatamu na Taasisi hiyo imeendelea kufanya mabadiliko ili
kuendana na hali hiyo.
Taasisi
ya MOI na Hospitali ya BLK ya India zilianzisha ushirikiano mwaka 2016
na hii ni mara ya pili kwa wataalamu kutoka hosipitali hizi kufanya
upasuaji kwa kushirikiana.