Chege Chigunda amekanusha vikali tuhuma zilizotokana na kusambaa kwa picha akiwa jukwaani na huku mkononi mwake (karibuni na kwapa) akiwa na kitambaa cheusi ambacho baadhi ya watu wanahisi ni hirizi.
Mtu wa kwanza kuikuza picha hiyo na kuandika kuwa ana mashaka kuwa kitambaa hicho huenda kikawa hirizi, ni Maimartha Jesse.
“Angalia mkono wa kushoto wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ?
any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata
ukiniroga saw a Tu…japo cna imani hiyoo,” aliandika mtangazaji huyo wa
zamani wa EATV.
Kauli hiyo ya Maimartha ilimfanya Chege kuamua kutoa ufafanuzi.
